Ukosefu wa ajira wakithiri Ugiriki

Imebadilishwa: 11 Oktoba, 2012 - Saa 15:38 GMT


Maafisa nchini Ugiriki wanasema kiwango cha ukosefu wa ajira nchini humo kilizidi asilimia ishirini na tano.

Kiwango hicho kiliongezeka kwa asilimia saba katika miezi kumi na miwili mfululizo na sasa kiko juu sawa na kilivyo nchini Hispania.

Mwandishi wa BBC anasema ongezeko hilo la ukosefu wa ajira ni kutokana na ukweli kwamba Ugiriki imekuwa katika kipindi cha mdororo wa uchumi kwa miaka mitano mfululizo.

Amesema hatua za kunusuru uchumi wa taifa hilo ambazo zimesababisha watu wengi kuachishwa kazi katika sekta ya umma na binafsi ni sababu ya ukosefu wa ajira nchini Ugiriki kuwa mbaya zaidi.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.