Kiongozi wa mashtaka afutwa kazi Misri

Imebadilishwa: 12 Oktoba, 2012 - Saa 08:54 GMT

Rais Mohammed Morsi

Rais wa Misri Mohammed Morsi, amemfuta kazi mwendesha mkuu wa mashtaka Abdel Meguid Mahmud.

Hatua ya rais imejiri siku moja baada ya mahakama nchini humo kutupilia mbali kesi za washirika wakuu wa Hosni Mubarak, ambaye alituhumiwa kwa mashambulizi dhidi ya waandamanaji wakati wa mapinduzi ya kiraia mwaka jana.

Lakini bwana Mahmoud aliwaambia waandishi wa habari kuwa Rais hana mamlaka kumfuta kazi, na kwamba hatajiuzulu.

Raia wengi wa Misri walimtuhumu bwana Mahmoud kwa kuwasilisha kesi zenye udhaifu sana dhidi ya washirika wa Mubarak, na kutowachukulia hatua kali za kisheria.

Miongoni mwa walioachiliwa ni maspika wawili wa zamani wa bunge , mawaziri na wafanyabiashara.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.