Malala kupata matibabu zaidi Uingereza

Imebadilishwa: 15 Oktoba, 2012 - Saa 14:20 GMT

Msichana mdogo wa Kipakistan Malala Yusufzai aliyepigwa risasi kichwani na Taliban baada ya kufanya kampeni kutetea haki ya elimu kwa wasichana, anatarajiwa kuwasili nchini Uingereza kwa matibabu.

Atakapowasili atapelekwa katika hospitali ya Birmingham ambako maafisa wa Pakistan wamesema atahitaji kufanyiwa upasuaji kurekebisha sehemu za fuvu la kichwa zilizoharibika na baadaye kupatiwa ushauri wa kisaikolojia.

Waziri wa Mambo ya nje wa Uingereza William Hague amesema Malala anahitaji matibabu maalum ambayo serikali ya Uingereza imeahidi kutoa.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.