Polisi wasitisha mgomo Afrika Kusini

Imebadilishwa: 16 Oktoba, 2012 - Saa 10:57 GMT

Polisi nchini Afrika Kusini wanasema kuwa wamesitisha mgomo wa wachimba migodi uliofanywa kinyume na sheria katika mgodi wa madini ya chuma katika mkoa wa Northern Cape.

Polisi waliwakamata takriban wachimba migodi arobaini na kudhibiti mashine kubwa ambazo walikuwa wameziiba kutoka kwa mgodi huo wa Sishen.

Ni mojawapo ya machimbo makubwa yaliyo wazi kote duniani.

Mnamo siku ya Jumatatu, zaidi ya wachimba migodi miamoja waliokuwa wanagoma walifutwa kazi na kampuni ya madini ya Anglo-American.

Sekta ya madini nchini Afrika Kusini, imeathiriwa vibaya sana na migomo ya wachimba migodi wanaodai mishahara mizuri na mazingira bora ya kazi.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.