Senegal nje ya kombe la taifa bingwa Afrika

Imebadilishwa: 17 Oktoba, 2012 - Saa 09:50 GMT

Senegal imetupwa nje ya kinyang'anyiro cha kuwania kombe la taifa bingwa barani Afrika

Tangazo hilo, linajiri baada ya shirikisho la soka barani humo kuipa ushindi wa mabao mawili Ivory Coast kufuatia vurugu za siku ya Jumamosi zilizosababishwa na mashabiki wa Senegal

Vurugu hizo zilisababisha kufutiliwa mbali kwa mechi kati ya nchi hizo mbili wakati Ivory Coast ikiwa na mabao mawili bila dhidi ya Senegal katika uwanja wa Dakaar.

Ivory Coast sasa itashiriki katika michuano ya kuwania kombe hilo itakayofanyika nchini Afrika Kusini mwezi Januari

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.