Iran taabani baada ya kuongezwa vikwazo

Imebadilishwa: 16 Oktoba, 2012 - Saa 14:50 GMT

Iran huenda ikajikuta katika hali mbaya zaidi baada ya Jumuiya ya Ulaya kuongeza vikwazo zaidi kwa karibu sekta nzima ya mafuta na gesi nchini Iran kutokana na mpango wake wa nuklia.

Maeneo yaliyolengwa na vikwazo hivyo ni pamoja na mradi wa taifa wa mafuta, makampuni ya kuzalisha gesi, wizara za nishati na petroli na makampuni yanayoshughulikia usafishaji, usambazaji na usafirishaji wa mafuta.

Hapo jana Jumuiya ya Ulaya iliongeza pia vikwazo vikali zaidi kwa Iran katika sekta ya benki na usafiri wa baharini.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Iran Ramin Mehmanparast ameshutumu uamuzi huo wa jumuiya ya Ulaya.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.