Upinzani uliwaua wafuasi wa Gadaffi

Imebadilishwa: 17 Oktoba, 2012 - Saa 11:12 GMT

Shirika la kutetea haki za binadamu Human Rights Watch limeshutumu wapiganaji nchini Libya kwa kuwaua zaidi ya watu sitini wanaoaminiwa kuwa wafuasi wa hayati Kanali Muamar Gadaffi .

Mauaji hayo inaaminika yalifanywa saa chache tu baada ya kukamatwa na kuuawa kwa kiongozi huyo.

Kundi hilo linasema kuwa wapiganaji hao waliwavamia watu hao katika hoteli moja mjini Sirte muda mfupi baada ya msafara wa Gadaffi kuvamiwa.

Kwa mujibu wa ripoti ya Human Rights Watch, mmoja wa wanawe Gadaffi, Mutassim aliuawa baada ya kupelekwa mjini Misrata.

Sasa shiriki hilo linataka serikali ya Libya kuchunguza mauaji hayo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.