Ripoti ya Israel kuhusu Gaza yafichuliwa

Imebadilishwa: 17 Oktoba, 2012 - Saa 13:18 GMT

Mahakama nchini Israel imelazimisha serikali kutoa ripoti yake kuhusu matumizi ya chakula katika ukanda wa Gaza.

Ripoti hiyo kwa jina "The Red Lines", ni matokeo ya utafiti uliofanywa na Israel miaka minee iliyopita wakati ilipoweka vikwazo dhidi ya kuingiza chakula na bidhaa zinginje katika ukanda wa Gaza kwa sababu za kiusalama.

Aidha ripoti hiyo inadokeza viwango vya kalori au uzio wa joto vilivyohitajika na wapalestina ili kuzuia utapiamlo.

Afisaa mmoja wa serikali ya Israel amesema kuwa ripoti hiyo ilikuwa tu rasimu na kwamba ilinuiwa kuhakikisha kuwa hapatokei mzozo wa kibinadamu katika eneo la Gaza.

Maafisa wa serikali ya Israel wanasema kuwa vikwazo hivyo vililenga kushinikiza kundi la Hamas kusitisha harakati zake kwa kufanya maisha ya watu Gaza kuwa magumu kiasi hicho.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.