Kaburi la hayati Arafat kufukuliwa

Imebadilishwa: 17 Oktoba, 2012 - Saa 11:01 GMT

Wendesha mashtaka wanaochunguza kifo cha aliyekuwa kiongozi wa Palestina Yasser Arafat nchini Ufaransa, watawasili mjini Ramallah ,katika Ukingo wa Magharibi mwezi ujao kulifukua kaburi la Arafat.

Wachunguzi watafukua kaburi la Arafat ili kuifanyia uchunguzi wa kisayansi maiti yake.

Majasusi kutoka nchini humo tayari, wamemuhoji mjane wake Suha mjini Paris, ambaye anaamini kuwa alipewa sumu.

Ufaransa ilianzisha uchunguzi katika mauaji hayo mwezi Agosti baada ya wataalamu nchini Uswizi, kupata chembechembe za sumu aina ya (Polonium) kwenye nguo zake.

Arafat alifariki katika hospitali moja mjini Paris miaka minane iliyopita.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.