Wauawa kwa kukatwa koo Indonesia

Imebadilishwa: 17 Oktoba, 2012 - Saa 10:15 GMT

Maiti za maafisa wawili wa polisi waliokuwa wanachunguza washukiwa wa siasa kali za kiisilamu, imepatikana huku koo zao zikiwa zimekatwa.

Msemaji wa polisi alisema kuwa wawili hao walikuwa na alama za kuteswa kabla ya kuuawa.

Walikuwa wanachunguza kambi moja katika eneo la Sulawesi, ambapo wapiganaji wa kiisilamu walishukiwa kutoa mafunzo. Polisi hao walipotea mapema mwezi huu.

Kundi la wapiganaji la, Jemaah Anshorut Tauhid,limelaumiwa kwa kufanya mauaji hayo ingawa msemaji wa kundi hilo amekana kuhusika kwao.

Polisi wamekuwa wakihusika na kampeini dhidi ya makundi ya wapiganaji wa kiisilamu waliofanya mashambulizi mabaya zaidi ikiwemo yale yaliyofanyika mjini Bali mwaka 2002.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.