Mkutano wa FARC na serikali ya Colombia

Imebadilishwa: 18 Oktoba, 2012 - Saa 12:32 GMT

Serikali ya colombia inafanya mashauriano ya amani na waasi wa FARC katika mji mkuu wa Norway, Oslo katika jaribio la kumaliza vita vya zaidi ya miongo mitano.

Mazungumzo hayo ni ya faragha lakini makundi hayo yatafanya mkutano na wanahabari hapo baadaye.

Maswala nyeti ni pamoja na ulanguzi wa mihadarati, ugavi wa ardhi na jukumu la kisiasa la baadaye la kundi hilo la waasi la mrengo wa kushoto.

Baada ya mazungumzo ya Norway, wataelekea katika mji mkuu wa Cuba, Havana kwa mazungumzo zaidi.

Serikali ya Colombia imesema vita havitasitishwa hadi waafikiane.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.