Mhariri wa BBC mashakani kuhusu kashfa ya kimapenzi

Imebadilishwa: 22 Oktoba, 2012 - Saa 15:19 GMT

Mhariri mkuu wa kipindi maarufu cha BBC ,NEWS NIGHT ameng'atuka uongozini ili kutoa nafasi kwa uchunguzi kufanyika wa kashfa ya kimapenzi na unyanyasaji wa kimapenzi wa watoto uliofanywa na aliyekuwa mtangazaji wa BBC Jimmy Savile.

Taarifa kutoka BBC imesema mhariri huyo Peter Rippon ametoa sababu zisizoridhisha za kuelezea kwanini alikataa kupeperusha makala ya uchunguzi iliyohusu madai ya jinsi mtangazaji Jimmy Savile alivyowanyanyasa watoto kimapenzi.

Tangu BBC ikatae kuonyesha ripoti hiyo , shirika lengine la Televisheni limeonyesha taarifa zinazodai kuonyesha jinsi mtangazaji huyo alivyoendesha kashfa hizo.

Hata hivyo BBC yenyewe imeanzisha uchunguzi kuhusu kashfa hiyo nzima.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.