''Polisi walitumia nguvu kupita kiasi Marikana''

Imebadilishwa: 22 Oktoba, 2012 - Saa 16:16 GMT

Baadhi ya wachimba migodi waliokuwa wamegoma

Polisi nchini Afrika Kusini wameelezea masikitiko yao kuhusu mauaji ya wachimba migodi 34 mnamo mwezi Agosti.

Wamesema kuwa huenda walitumia nguvu kupita kiasi. Ushahidi huu umetolewa katika tume inayochunguza mauaji ya Marikana ambapo Polisi walihusika.

Wakili wa polisi Ishmail Semenya aliambia tume hiyo kuwa walishindwa kudhibiti hali wakati wakijaribu kuwatawanya waandamanaji elfu tatu.

Alisema kuwa polisi waliwafyatulia risasi waandamanaji kumi na sita bila ya amri yoyote kufanya hivyo na kisha kuwafuata wachimba migodi wengine kumi na wanane waliosalia na kuwapiga risasi.

Tume hiyo ilirejelea vikao vyake leo baada ya kuvisitisha mapema mwezi huu ili kuruhusu familia za wale waliofariki wakati wa vurugu za Marikana kusafiri kwenda kusikiliza vikao hivyo.

Wengi wao wanaishi mamia ya kilomita mbali na ambako tume hiyo inaendesha vikao vyake.

Mnamo mwezi Agosti Polisi iliwafyatulia risasi waandamanaji katika mgodi huo na kuwaua wachimba migodi 34,baada ya vurugu kuzuka katika maandamano hayo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.