Kimbunga Sandy chaleta uharibifu visiwani

Imebadilishwa: 25 Oktoba, 2012 - Saa 08:00 GMT


Kimbunga cha Sandy kimekumba nchi ya Jamaica na kusababisha uharibifu mkubwa.

Kituo cha runinga cha nchi hiyo kinasema kuwa asili mia 70 ya kisiwa hicho hicho hakuna umeme baada ya mvua kubwa na dhoruba kali kuangusha miti na milingoti ya stima.

Wakaazi wanashauriwa kusalia nyumbani na amri ya kutoka nje imewekwa ili kuzuia uporaji.

Kwa sasa kimbunga hicho kinakaribia mashariki ya Cuba moja ya sehemu ambayo watabiri wa hali ya anga walikuwa wametahadharisha.

Kimbunga hicho vile vile kinatarajiwa kuelekea maeneo ya Bahamas na huenda Florida pia.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.