Hoja ya msaada wa Uingereza kwa Afghanistan

Imebadilishwa: 25 Oktoba, 2012 - Saa 08:34 GMT

Kundi la wanasiasa kutoka Uingereza wanaosimamia maswala ya msaada unaotolewa na nchi hiyo kimataifa, wamesema kuwa Uingereza inatakiwa kuelewa kuwa ni vigumu kuwa na serikali thabiti nchini Afghanistan.

Kamati hiyo ya maendeleo ya kimataifa imesema kuwa uingereza inatakiwa kukoma kufadhili taasisi mbalimbali za serikali ya Agfhanistan wakati mataifa mengine yanaondoa huko vikosi vyao vya usalama.

Wabunge hao badala yake wamesema Uingereza inatakiwa kuboresha maisha ya wanawake nchini Afghanistan ambao wanakabiliwa na umasikini mkubwa.

Uingereza hutoa msaada wa dola milioni 290 kila mwaka kwa Afghanistan

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.