Jarida lafungwa kwa ufichuzi China

Imebadilishwa: 26 Oktoba, 2012 - Saa 09:39 GMT

Gazeti la New York Times limesema kuwa tovuti yake imefungwa nchini China baada ya kuchapisha taarifa ya uchunguzi kuhusu jamaa za waziri mkuu wa Uchina, Wen Jiabao.

Gazeti hilo liliripoti kuwa familia ya Bwana Wen inamiliki mali ya thamani ya dola bilioni mbili nukta saba lakini hakuna ithibati kuwa Wen anajihusisha na biashara za familia yake.

Gazeti hilo limeongeza kuwa Uchina inapinga vikali ripoti hiyo iliyotakiwa kuchapishwa katika shirika moja maarufu la kutoa huduma za Blogu.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje alisema kuwa ripoti hiyo iliiweka dosari serikali ya China na kuwa ilifanywa kwa nia mbaya.

Taarifa zozote kuhusu bwana Wen na familia yake zimebanwa katika mitandao maarufu ya China.

Gazeti hilo lilisema kuwa mkewe Wen, mamake na mwanao , walijipatia mali nyingi baada ya waziri mkuu huyo kuimarika kisiasa.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.