Mashakani kwa kumpinga Rais Putin

Imebadilishwa: 26 Oktoba, 2012 - Saa 13:03 GMT

Mwanaharakati wa upinzani nchini Urusi Sergei Udaltsov, ameshtakiwa kwa kujaribu kupanga maandamano dhidi ya Rais Vladimir Putin.

Mwanaharakati huyo mashuhuri ambaye bado hajakamatwa ingawa anakabiliwa na vikwzo vya usafiri, huenda akafungwa jela miaka kumi ikiwa atapatikana na hatia.

Bwana Udaltsov aliambia waandishi wa habari mjini Moscow kuwa hana hatia ya kosa lolote

Kipindi kimoja kilichopeperushwa kwa televisheni mapema mwaka huu, kilidai kuwa alikuwa na njama ya kupanga maandamano dhidi ya serikali kwa kutumia pesa kutoka kwa mbunge mmoja wa Georgia.

Washukiwa wenzake wawili wameshtakiwa akiwemo mmoja aliyesema alikamatwa na maafisa wa Urusi nchini Ukrain.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.