Vita nchini Syria licha ya makubaliano

Imebadilishwa: 26 Oktoba, 2012 - Saa 13:22 GMT

Kumetokea vurugu katika sehemu kadhaa za Syria licha ya makubaliano ya kusitisha vita kati ya serikali na waasi.

Wanaharakati wanasema kuwa watu kumi wameripotiwa kufariki huko Damascus, Homs na karibu na mji wa Maaret al-Numan.

Mapatano ya kusitisha Mapigano kwa muda yalikuwa yamependekezwa na mpatanishi wa umoja wa mataifa ili kuwaruhusu wasyria waadhimishe siku kuu ya Eid ul Adha hii leo

Makundi ya kutoa misaada yamethibitisha mapigano makali katika sehemu nyingi za nchi hiyo.

Makundi hayo yalikuwa yananuia kufaidi kuwepo kwa amani katika sherehe za sikukuu ya Eid ili kuweza kutoa misaada ya Chakula na dawa katika maeneo ya Aleppo yaliyokuwa yamekumbwa na vita katika siku za hivi karibuni.

Waandamanaji wa upinzani walitumia fursa ya kupungua kwa ghasia hata hivyo kufanya mikutano ya hadhara baada ya sala aya Ijumaa.

Mashirika ya misaada yanatumai kuwa hali itatulia ili yawezea kutoa misaada zaidi.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.