Kimbunga tisho kwa watu milioni hamsini

Imebadilishwa: 29 Oktoba, 2012 - Saa 14:34 GMT

Wataalamu wa utabiri wa hali ya hewa nchini Marekani wameonya kuwa kimbunga Sandy ni tisho kubwa kwa takribani watu millioni hamsini katika Pwani ya Mashariki nchini humo ambako idadi kubwa ya watu wanaishi.

Wamesema kuwa mji wa New York huenda ukaathirika zaidi kwa kuwa unazungukwa na maji.

Awali meya wa NewYork, Michael Bloomberg aliagiza kuhamishwa kwa watu takriban laki tatu na elfu sabini wanaoishi katika sehemu za chini kwenye eneo hilo.

Soko la hisa la New York limefungwa na zaidi ya ndege elfu tano zilisitisha safari zao.

Huduma za usafiri wa basi na reli zimesitishwa na shule zimefungwa leo huku wafanyakazi wa serikali wasiofanya katika taasisi za huduma ya dharura mjini Washington wakiambiwa wasiende kazini.

Naye Rais Barack Obama amewaonya raia nchini Marekani kukichukulua kimbunga Sandy kwa uzito wakati kikikaribia mashariki ya pwani ya nchi hiyo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.