Rais wa zamani Ufilipino mahakamani

Imebadilishwa: 29 Oktoba, 2012 - Saa 07:41 GMT

Rais wa zamani wa Ufilipino, Gloria Arroyo, amefikishwa mahakamani kwa mashtaka ya kutumia vibaya kima cha dola milioni tisa pesa za serikali za mchezo wa bahati nasibu zilizonuiwa kuwasaidia watu kwa maslahi yake.

Arroyo alikataa kujibu mashtaka kwa hiyo mahakama ikanukuu kwa niaba yake, kuwa amekana mashtaka hayo.

Ni kesi ya tatu ya rushwa dhidi ya rais huyo wa zamani wakati alipokuwa kiongozi. Amekana mashtaka yote na anamshutumu kiongozi aliyemrithi, Benigno Aquino, kuanzisha kisasi dhidi yake.

Alifikishwa mahakamani kutoka hospitali ya kijeshi ambako alikuwa amelazwa siku kadhaa kabla ya kupewa kwa mara ya kwanza waranti iliyotolewa ya kumkamata.

Anasemekana kuwa na matatizo ya shingo na alifika mahakamani akiwa amevalia bendeji shingoni.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.