Makao ya Scotland Yard kuuzwa

Imebadilishwa: 30 Oktoba, 2012 - Saa 15:21 GMT

Makao makuu maarufu ya kikosi cha Polisi wa Ujasusi cha New Scotland Yard, yatauzwa katika mpango kabambe wa kupunguza gharama.

Idara ya Polisi imesema inatarajiwa kuokoa zaidi ya dola milioni kumi kila mwaka kwa kuhamia kwenye makao madogo.

Jumba hilo limekuwa makao makuu ya Polisi kwa muda wa miaka arobaini na tano, huku kikosi hicho hapo awali kikitumia makao mengine katikati mwa Jiji la London yanayojulikana kama Scotland Yard tangu karne ya kumi na tisa.

Idara ya Polisi inapanga kutumia pesa ilizookoa katika mpango huo kulipia maafisa zaidi wa Polisi wanaopiga doria.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.