Aliyekuwa mkuu wa jeshi Serbia, kukata rufaa

Imebadilishwa: 30 Oktoba, 2012 - Saa 10:09 GMT

Aliyekuwa mkuu wa zamani wa jeshi nchini Serbia, Momcilo Perisic, anatarajiwa kufika mahakamani leo mjini Hague Uholanzi kukata rufaa kupinga hukumu iliyotolewa dhidi yake ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binaadamu, wakati wa mzozo uliokuwepo katika iliyokuwa Yugoslavia.

Perisic amepewa dakika kumi kujitetea dhidi ya hukumu hio na kifungo cha miaka 27 gerezani aliyopewa na mahakama mnamo mwaka 2011.

Anasisitiza hakujuwa wala kuhusika kwa maovu yakiwemo mpango wa kushambulia na kuwafyatulia risasi wakaazi wa mji mkuu wa Bosnia, Sarajevo.

Waserbia wengine waliokuwa wakuu nchini humo, Radovan Karadzic, Ratko Mladic and Goran Hadzic pia watafika mbele ya jopo la mahakama, kwa mara ya kwanza, wote kufika kwa pamoja.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.