Utata wa bwawa kati ya Laos na Vietnam

Imebadilishwa: 5 Novemba, 2012 - Saa 15:41 GMT

Serikali ya Laos imetangaza kuwa itaendelea na mpango wake tatanishi wa kujenga bwawa la kwanza katika eneo la chini la mto Mekong.

Uamuzi wa kujenga bwawa hilo kwa jina maarufu Xayaburi umetolewa licha ya kuwepo malalamiko ya wanaharakati wa kuhifadhi mazingira na mataifa yalio katika eneo hilo.

Cambodia na Vietnam zina wasiwasi kuwa bwawa hilo lenye thamani ya dola bilioni tatu na nusu litaharibu idadi ya samaki na kuwa na athari mbaya kwa usalama wa chakula kwa mamilioni ya watu.

Tangazo hili lilitolewa siku ambayo viongozi kutoka Asia na Ulaya walianza mkutano wa siku mbili katika mji mkuu wa Laos Vientiane.

Mpango wa maendeleo wa taifa la Laos ambalo ni taifa maskini katika rasi ya kusini mashariki mwa Asia, unahusisha kutengeneza umeme kutoka mito yake na kuuza nishati hiyo kwa majirani wanaozidi wa taifa hilo.

Uamuzi huu wa ujenzi katika eneo hilo la Xayaburi unajiri licha ya kuwepo wito kutoka mataifa yalio katika eneo la chini kusitisha mradi huo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.