Shambulizi la kigaidi latokea Bahrain

Imebadilishwa: 5 Novemba, 2012 - Saa 14:47 GMT

Mabomu kadhaa madogo yamelipuka katika mji mkuu wa Bahrain Manama, na kusababisha vifo vya wafanyakazi wawili wa mataifa ya kigeni na kumjeruhi mmoja.

Maafisa wa serikali wanasema milipuko hiyo ilisababishwa na mabomu matano yaliyotengenezwa nyumbani.

Shirika la kitaifa la habari lilieleza milipuko hiyo kuwa shambulizi la kigaidi.Lilisema kuwa waathiriwa ni raia wa kutoka Asia.

Watu sitini wameuawa katika machafuko yanayoendelea nchini Bahrain yaliyoanza kutokana na maandamano ya kuunga mkono mageuzi mnamo mwezi Februari mwaka jana na yalizimwa na vikosi vilivyokuwa vimejihami.

Katika wiki za hivi karibuni maafisa wawili wa polisi wameuawa baada ya kupata majereha kutokana na milipuko hiyo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.