Makosa dhidi ya jaji mkuu wa Sri Lanka

Imebadilishwa: 6 Novemba, 2012 - Saa 12:42 GMT

Serikali ya Sri Lanka imechapisha maelezo ya mashtaka dhidi ya jaji mkuu wa nchi hiyo.

Anatuhumiwa kwa kukosa kuweka wazi mapato yake na mali yake yote katika juhudi za kupiga kura ya kutokuwa na imani naye.

Jaji Shirani Bandaranayake mwanamke wa kwanza kuwahi kuwa jaji mkuu nchini humo, anatuhumiwa kwa kutumia vibaya mamlaka yake na kuipa sifa mbaya ofisi yake.

Wakosoaji wanasema kuwa hatua hiyo inanuia kukandamiza uhuru wa mamlaka.

Inafuatia wiki kadhaa za mgogoro kati ya Rais Mahinda Rajapaksa na idara ya mahakama.

Mnamo siku ya Jumatatu, zaidi ya watu elfu moja wengi wakiwa mawakili walifanya maandamano dhidi ya serikali mjini, Colombo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.