Wakuu wa jeshi kizimbani Uturuki

Imebadilishwa: 6 Novemba, 2012 - Saa 12:22 GMT

Kesi inaendelea nchini Uturuki hii leo dhidi ya wakuu wa jeshi waliostaafu, pasina wao kuwepo mahakamani.

Wanashutumiwa kwa kupanga uvamizi wa meli ya Uturuki iliyojaribu kuvunja vikwazo ilivyoweka Israel kuzuia meli kuingia katika ukanda wa Gaza.

Wanaharakati tisa, wengi wao raia wa Uturuki waliuawa wakati makomando wa Israeli walipoivamia meli hiyo waliokuwemo, (MAVI Marmara), mnamo Mei mwaka 2010.

Uturuki iliishutumu Israeli kwa kutekeleza ugaidi wa kitaifa lakini serikali ya Israeli inasisitiza kuwa makomando wake walichukua hatua hiyo ili kujikinga.

Shambulio hilo liliharibu vibaya uhusiano wa karibu uliokuwepo kati ya nchi hizo mbili.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.