Changamoto ya kupunguza matumizi Ugiriki

Imebadilishwa: 6 Novemba, 2012 - Saa 11:58 GMT

Mgomo wa siku mbili wa kupinga hatua kali za kubana matumizi, umesitisha usafiri na huduma nyengine nchini Ugiriki.

Wafanyakazi wanalalamika dhidi ya mpango wa kuokoa dola bilioni kumi na tatu na kupandishwa kodi ikiwa ni mapendekezo yaliyotolewa na serikali.

Mwandishi wa BBC aliye mjini Athens anasema hasira inazidi miongoni mwa wananchi walnaohisi kuchoshwa, lakini serikali inasema ni muhimu kuchukua hatua za kupunguza matumizi iwapo nchi hiyo inataka kuepuka kufilisika.

Hata hivyo mwandishi wa BBC anaongeza kwamba hata iwapo mapendekezo hayo hayataidhinishwa bungeni hapo kesho jumatano, deni la serikali litazidi mwaka ujao kufika kiwango kisichoweza kuhimiliwa na kuwa mara mbili ya matumizi ya serikali.

Mapendezekezo ya hivi karibuni ya bajeti hiyo ni sharti yatekelezwe kwa nchi hiyo ili iweze kupata awamu nyengine ya mkopo wa kimataifa.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.