Afungwa miaka 16 kwa ubakaji Afghanistan

Imebadilishwa: 7 Novemba, 2012 - Saa 11:38 GMT

Afisaa mmoja wa polisi nchin Afghanistan amehukumiwa kifungo cha miaka 16 gerezani kwa kumbaka msichana mwenye umri wa miaka kumi na nane.

Msichana huyo alitekwa nyara na kundi la maafisa wa polisi wa Afghanistan na baadaye alipigwa na kubakwa katika kipindi cha siku tano mnamo mwezi Mei mwaka huu.

Waandishi habari wanasema kesi hiyo siyo ya kawaida kwa kuwa mwanamke huyo ndiye aliyeripoti kisa hicho.

Vyombo vya habari vya kimataifa vimeangazia mashtaka yake na kumfanya rais Karzai kuagiza uchunguzi wa uhalifu. Maafisa wengine watatu wa polisi pia walihukumiwa kwa kuhusika na ubakaji huo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.