Wanaharakati wapokonywa uraia Bahrain

Imebadilishwa: 7 Novemba, 2012 - Saa 11:44 GMT

Maafisa wa serikali nchini Bahrain wamewapokonya uraia wanaharakati thelathini na mmoja wa madhehebu ya kishia, wawili kati yao walikuwa wabunge walioliwakilisha kundi kuu la Shia Al-Wefaq.

Sheria ya uraia nchini Bahrain inaruhusu ukaguzi wakati serikali inaona kuwa raia anatatiza usalama wa taifa.

Taarifa kutoka wizara ya mambo ya ndani imesema watu hao wana haki ya kukata rufaa.

Makundi ya kutetea haki za binaadamu nchini Barain yana wasiwasi kuhusu uamuzi huo yakisema kuwa serikali haikutoa ushahidi wa kutosha kuhusu kwanini watu hao wamepokonywa uraia.

Hatua hiyo ya serikali inajiri baada ya Bahrain kupiga marufuku maandamano na mikutano yote ya hadhara kwa kigezo cha kuhofia usalama.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.