Kimbunga chasababisha uhaba wa umeme Cuba

Imebadilishwa: 8 Novemba, 2012 - Saa 13:58 GMT

Wiki mbili baada ya kimbunga Sandy kutokea nchni Cuba mji wa pili katika kisiwa hicho Santiago unakabiliana na tatizo la kurudisha huduma ya nishati ya umeme kwa wakaazi wa eneo hilo.

Makadirio ya awali nikuwa nyumba zilizoharibiwa kutokana na n kimbunga hicho ni takriban laki mbili, huku shule, hospitali na mashamba ya ukulima yakiwa yameathirika pia.

Usaidizi wa kibinaadamu umekuwa ukiwasilishwa katika kisiwa hicho hususan kutoka Venezuela, na raia wa Cuba walioko katika eneo la Magharibi mwa kisiwa hicho wamekuwa wakitoa misaada kwa walioathirika katika eneo la Mashariki.

Jorge na Mariela, ni wakaazi katika eneo hilo la Santiago, wanasema ni kimbunga kibaya ambacho hawajahi kukishuhudia katika eneo hilo.Jorge anasema mambo ni mabaya mno. Hakuna maji, hakuna umeme, kwa takribani wiki mbili sasa.

Shirika la chakula la Umoja wa mataifa, WFP, sasa linawasaidia wanaotaka kusafirisha misaada hadi nchini Cuba. Nchi ambayo inang'ang'ana kuinua uchumi wake hata kabla ya kuathirika na kimbunga hicho.

Kwa sasa chakula na vifaa vya ujenzi vimeanza kuwasili kutoka nchi za nje.

Na katika mji wa Santiago, wafanyakazi wa kusafisha mji wameanza kazi, barabara kuu imesafishwa na wanafunzi wamerudi shuleni. Wataalamu wanawasili kutoka maeneo yote ya Cuba kusaidia katika jitihada kubwa za kuirudisha hali nchini kama ilivyokuwa.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.