HSBC mashakani kwa kutolipa kodi

Imebadilishwa: 9 Novemba, 2012 - Saa 12:13 GMT

Halmashauri ya ushuru nchin Uingereza inachunguza mojawapo ya kubwa duniani HSBC kufuatia tuhuma kutoka kwa wateja wake kuwa imekwepa kulipa kodi.

Gazeti la kila siku Uingereza The Daily Telegraph limesema limepokea taaarifa kuhusu akaunti za zaidi ya wateja elfu nne wa Uingereza zilizopo nje ya nchi hiyo katika kisiwa cha Jersey.

Gazeti hilo linaripoti kuwa majina hayo ni pamoja na mfanyabiashara mkuu wa madawa ya kulevya, muuzaji silaha, na watu wengine wenye rekodi mbaya ya uhalifu.

Benki hiyo imesema inachunguza ripoti hizo, lakini haijajulishwa kuhusu uchunguzi wowote unaofanyika.

Mwandishi wa masuala ya biashara wa BBC amesema tuhuma hizo zinazusha maswali muhimu kuhusu uwezo wa benki hiyo kukagua wateja wake.

Kwa sasa HSBC inakabiliwa na uchunguzi wa kando nchini Marekani kuhusu tuhumu za kujipatia fedha kwa njia haramu.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.