Wanajeshi wa Marekani waadhibiwa

Imebadilishwa: 9 Novemba, 2012 - Saa 12:25 GMT

Wanajeshi saba wamarekani wa kitengo cha Elite akiwemo mmoja wa maafisa wa jeshi aliyehusika na kumkamata na kumuua Osama bin Laden wameadhibiwa kwa madai ya kutoa taarifa za siri za marekani kinyume na sheria.

Kuvunjwa kwa usalama huo kunadaiwa kujiri wakati wanajeshi hao walikuwa wakifanya kazi ya kutoa huduma za ushauri katika kutengeneza mchezo wa video inayoonyesha makabiliano ya kijeshi.

Saba hao walipata barua za nidhamu na kupokea nusu ya mishahara yao kwa kipindi cha miezi miwili .

Idara ya usalama ya marekani bado inachunguza iwapo maafisa zaidi wa kitengo cha Seal walihusika

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.