Tetemeko la ardhi laitingisha Guatemala

Imebadilishwa: 12 Novemba, 2012 - Saa 07:58 GMT

Tetemeko kubwa la ardhi limeitingisha nchi ya Guatemala siku chache tu baada ya takriban watu 52 kuuwawa na tetemeko kubwa zaidi kuonekana katika miongo kadhaa iliyopita.

Kiini cha tetemeko hilo, liliokuwa na nguvu ya Richter ya 6.2, kilikuwa umbali fulani kutoka pwani ya Guatemala katika Bahari ya Pacific, na lilisikika pia nchini El Salvador, na jimboni Chiapas, nchini Mexico.

Kwa sasa, hakuna ripoti za hasara yeyote kubwa, wala vifo, lakini tetemeko hili la pili kutokea chini ya juma moja limezua hofu nchini Guatemala.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.