Abu Qatada kuachiliwa kwa dhamana leo

Imebadilishwa: 13 Novemba, 2012 - Saa 09:38 GMT

Mhubiri wa Kiislamu mwenye itikadi kali Abu Qatada anatarajiwa kuwachiliwa kwa dhamana leo Jumanne baada ya kushinda kesi ya muda mrefu ya kupinga kuhamishwa kutoka Uingereza hadi Jordan anakotakikana kwa kupanga shambulio la bomu.

Ataachiliwa kutoka gerezani kwa vikwazo vya kutotoka nje kwa saa kumi na sita.

Dhamana hiyo ilitolewa na Tume maalum ya Uhamiaji iliyosema kuna hofu ya ushahidi uliokusanywa kupitia mateso, kutumika dhidi ya Abu Qatada nchini Jordan.

Wakili wa Abu Qatada Gareth Peirce, amesema ni haki kwa Uingereza kufuata sheria.

Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza Theresa May amesema atakata rufaa dhidi ya uamuzi huo. Waziri mmoja wa Jordan Nayef al Fayez pia ameiambia BBC kuwa nchi yake itaunga mkono rufaa hiyo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.