Aung San Suu Kyi ziarani India

Imebadilishwa: 13 Novemba, 2012 - Saa 13:22 GMT

Kiongozi wa Upinzani nchini Burma na mshindi wa Tuzo la Nobel Aung San Suu Kyi, anawasili nchini India leo Jumanne, kwa ziara yake ya kwanza kwa takriban miaka arobaine.

Jumatano, atatoa hotuba muhimu Mjini Delhi na kufanya mashauriano na viongozi wa kisiasa, akiwemo waziri Mkuu Manmohan Singh.

Aung San Suu Kyi aliishi nchini India miaka ya sitini, mamake alipokuwa balozi wa Burma nchini humo.

Wachanganuzi wanasema India inataka kuimarisha ushawishi wake Burma, nchi hiyo inapoendelea kujiweka wazi kwa uwekezaji kutoka nje.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.