Waasi tayari kwa mazungumzo Colombia

Imebadilishwa: 13 Novemba, 2012 - Saa 10:01 GMT

Kundi la pili kubwa zaidi la waasi nchini Colombia ELN, linasema liko tayari kushiriki mazungumzo ya amani na serikali.

ELN, ama jeshi la Kitaifa la Ukombozi, lilitangaza hayo kwenye tovuti yake, siku chache kabla ya kuanza kwa mazungumzo ya amani katika mji mkuu wa Cuba, Havana, kati ya serikali ya Colombia na wajumbe kutoka vikundi vikuu vya waasi, FARC.

Licha ya mazungumzo hayo kutarajiwa kuanza, mapigano yameendelea Colombia.

Nyumba kadhaa zimeharibiwa na zaidi ya watu ishirini kujeruhiwa katika mashambulio yanayoshukiwa kutekelezwa na FARC Kusini Magharibi mwa mji wa Suarez.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.