Wafungwa waachiliwa huru

Imebadilishwa: 14 Novemba, 2012 - Saa 13:42 GMT

Pakistan imekubali kuwaachilia huru wafungwa kadhaa wa taliban.

Maafisa wa serikali ya Afghanistan wametaja hatua hiyo iliyotangazwa wakati wa mazungumzo mjini Islamabad kama muhimu katika juhudi za kuleta amani.

Aidha waliiambia BBC, kuwa miongoni mwa walioachiliwa huru ni wafungwa maarufu, akiwemo waziri wa zamani wa Sheria wa Taliban, Mullah Turabi.

Mwandishi wa BBC mjini Islamabad anasema tumaini ni kuwa maafisa hao wa taliban watakaporejea nyumbani, wanaweza kuwashawishi wengine kushirikimazungumzo ya amani.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.