Uchina yapata kiongozi mpya

Imebadilishwa: 15 Novemba, 2012 - Saa 08:21 GMT

Imethibitishwa kwamba Xi Jinping ndiye atakayeongoza Uchina kwa mwongo ujao.

Bwana Li aliongoza Kamati ya Politburo kupanda jukwaa la Ukumbi Mkuu wa Wananchi mjini Beijing, ishara ya kwamba ndiye kiongozi mkuu wa chama tawala cha Uchina cha Kikomunisti.

Alisema kuwa ingawaje chama hicho kinakumbwa na changamoto nyingi, lakini kitajitahidi kukidhi "matarajio ya historia na ya wananchi".

Siasa za wanakamati wengi wa Politburo sio kali, na maoni ya wengi ni kwamba wanamageuzi wengi hawakupandishwa vyeo.

Xi Jinping anachukua mahali pa Hu Jintao. Chini ya utawala wa mwongo mmoja wa Hu Jintao Uchina ilikua kwa kasi sana kiuchumi.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.