Misri yashutumu mashambulizi ya Israel

Imebadilishwa: 15 Novemba, 2012 - Saa 10:19 GMT

Chama cha Uhuru na Haki, ambalo ni kitengo cha kisiasa cha Muslim Brotherhood huko Misri, kimelaani shambulizi la jeshi la anga la Israel lililomuua kiongozi wa kijeshi wa Hamas, Ahmed Al Jabari.

Aidha, kimesema kuwa kinaunga mkono kile kinachoona kuwa ni harakati za Wapelestina.

Kikitoa taarifa, chama hicho kilisema kuwa Misri haingekubali unyanyasaji na uchokozi wa Wapelestina unaofanywa na Waisraeli.

Wakati huo huo, Misri imetangaza kuwa itamrudisha nyumbani balozi wake aliyeko Israel kwa sababu ya mashambulizi ya nchi hiyo dhidi ya Gaza.

Rais Muhammad Morsi, akitoa taarifa katika runinga ya serikali, alisema Misri itamuita balozi wa Israel aliyeko Cairo ili apokee barua ya shutuma.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.