Uchumi wa Eurozone wadorora tena

Imebadilishwa: 15 Novemba, 2012 - Saa 12:08 GMT

Takwimu rasmi za hivi punde zinaonyesha kwamba uchumi wa eneo la Eurozone umeanza kudorora tena.

Shirika linalotoa huduma za takwimu barani Ulaya, Eurostat, limesema kuwa chumi za nchi za eneo hilo, lenye nchi 17, zilizorota kwa kiasi cha asilimia 0.1 kati ya Julai na Septemba, baada ya kudorora kwa asilimia 0.2 katika miezi mitatu iliyotangulia hapo.

Nchi zinazofanya vibaya zaidi ni Uhispania, Cyprus na Ugiriki – nchi ambazo zina matatizo makubwa kiuchumi.

Uchumi wa Ujerumani, ambao ndio mkubwa zaidi Eurozone, ungali unakua, ingawaje huathiriwa na tatizo sugu la madeni ya Eurozone.

Hali hii ya kudorora kwa chumi za eneo hilo imetokea miaka mitatu baada ya nchi hizo kukumbwa na hali hiyo hiyo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.