Baraza la mawaziri Ivory Coast lavunjwa

Imebadilishwa: 15 Novemba, 2012 - Saa 07:51 GMT

Rais wa Ivory Coast Alassane Outtara amelivunja baraza lake la mawaziri baada ya mzozo kuhusu sheria mpya ya ndoa itakayowapa wake haki sawa na waume zao.

Chama cha Ouattara kiliunga mkono sheria hii, lakini viongozi wa upinzani waliopo serikalini waliupinga.

Kama sheria nyingi barani Afrika, sheria za nchi hiyo kwa sasa humpa mamlaka zaidi mume, akiwa kiongozi wa familia, naye hupewa jukumu la kufanya uamauzi kuhusu maswala muhimu ya familia - jambo ambalo Ouattara anataka kubadlisha.

Juzijuzi, serikali ya Kenya ilipedekeza kufutiliwa mbali kwa ulipaji mahari, swala lililozua mjadala mkubwa.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.