Ugonjwa wa Ebola wazuka tena Uganda

Imebadilishwa: 15 Novemba, 2012 - Saa 09:27 GMT

Ugonjwa wa Ebola umezuka tena nchini Uganda miezi miwili tu baada ya nchi hiyo kuambiwa kuwa ugonjwa huo haupo tena.

Thibitisho hilo lilitolewa na Wizara ya Afya nchini, pamoja na Shirika la Afya Duniani.

Watu wawili wameshafariki baada ya kuugua ugonjwa huo huko Luweero, Uganda kati. Walikuwa wakaazi wa kijiji cha Kakuute, na walifariki baada ya kuvuja damu, kutapika, kuhisi maumivu kifuani, na homa.

Wakati huo huo, Uganda inaendelea kupambana na ugonjwa wa Marburg wilayani Kabale na maeneo jirani.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.