Maafisa wa polisi 2 wauawa Garisa

Imebadilishwa: 16 Novemba, 2012 - Saa 13:05 GMT
Afisa wa polisi aliyejeruhiwa Barogoi

Afisa wa polisi aliyejeruhiwa Barogoi

Maafisa wawili wa polisi wameuawa huko Garissa Kaskazini mwa Kenya kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana.

Kwa sasa wakuu wa serikali katika eneo hilo wanaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo lakini hawajatoa taarifa rasmi kuhusina na mauji hayo.

Mauaji hayo yanatokea siku chache baada ya maafisa wengine wa polisi wapatao 42 kuuawa na wezi wa Mifugo katika eneo la Kaskani Maghari mwa Kenya.

Mwandishi wa BBC anasema maafisa hao wa polisi walikuwa wakishika doria wakati watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki kuwavizia na kuwapiga risasi kabla ya kutoweka na silaha zao.

Maafisa hao waliaga dunia papo hapo na maafisa wa polisi wa kupambana na ugaidi na wale wa kawaida walifika katika eneo la tukio hilo na kwa sasa uchunguzi unaendelea lakini kuna fununu kuwa waliotekeleza mashambulio hayo ni watu wanaounga mkono wapiganaji wa Al shabaab.

Katika siku za hivi karibu kenya imeshuhudia mashambulio kama hayo, tangu wanajeshi wa Kenya kuingia nchini Somalia, kusaidia wanajeshi wa serikalio ya nchi hiyo kupambana na wapiganaji hao wa Al Shabaab.

Kwa sasa jeshi la Kenya likishirikiana na lile la Somalia wanathibiti mji wa Bandari wa Kismayo baada ya kuwatimua wapiganaji wa Al Shabaab, kutoka mji huo ambao ulikuwa ngome yao kuu.

wetu Bashkash Jugsday anaarifu kutoka ameneo hayo ya Garissa.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.