Muungano wa upinzani kuzuru London

Imebadilishwa: 16 Novemba, 2012 - Saa 10:55 GMT

Viongozi wa Muungano mpya wa upinzani nchini Syria watafanya mashauriano na serikali ya Uingereza jijini London leo Ijumaa, kwa imani kuwa watapata kutambuliwa rasmi.

Viongozi wa Uingereza wanatarajiwa kushinikiza muungano huo, kuweka wazi mpango wa mabadiliko ya kisiasa na serikali ya pamoja.

Uingerea pia inatafakari kutoa usaidizi kwa juhudi za Ufaransa za kuondoa vikwazo vya kutoawauzia silaha, waasi nchini Syria.

Ufaransaa ndio nchi ya kwanza ya Magharibi kutambua muungano huo kama waakilishi rasmi wa raia wa Syria.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.