Mzozo wa Israel na Gaza kutatuliwa-Mursi

Imebadilishwa: 18 Novemba, 2012 - Saa 13:20 GMT

Rais Mohamed Mursi wa Misri, amesema kuna ishara kuwa makubaliano ya kusitisha mapigano karibu yataafikiwa baina ya Israel na Wapalestina wa Gaza.

Rais Mursi amesema yamekuwako mawasiliano mengi baina ya pande hizo mbili, lakini hadi sasa hakuna thibitisho lolote.

Serikali ya Misri ndio makao ya juhudi nyingi za kidiplomasia kujaribu kumaliza mzozo huo.

Lakini mwandishi wa BBC mjini Cairo, anasema hakuna ishara halisi za kuonesha kuwa Israel au Hamas ziko tayari kuacha kupigana.

Jumuia ya nchi za Kiarabu inaunga mkono juhudi za Misri kupatanisha pande hizo mbili na inasema inapanga kutuma ujumbe katika eneo la Gaza siku chache zijazo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.