Meli ya Korea imekamatwa Somalia

Imebadilishwa: 18 Novemba, 2012 - Saa 13:25 GMT

Wakuu wa jimbo la Somalia lilojitenga, la Puntland, wanasema wameizuia meli ya Korea Kaskazini, kwa sababu ikimwaga saruji na vitu vengine baharini.

Wanasema wameikamata meli hiyo na mabaharia wake zaidi ya 30, karibu na bandari ya Bossasso.

Serikali ya Puntland inasema itawafikisha mabaharia hao mahakamani, kwa kosa la kuchafua mazingira.

Korea Kaskazini haikusema kitu hadi sasa.

Ripoti kuhusu meli kumwaga uchafu nje ya mwambao wa Somalia zimekuwa nyingi, kwa sababu kwa zaidi ya miongo miwili Somalia haikuwa na serikali yenye nguvu.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.