Serikali ya Colombia, waasi wajadiliana

Imebadilishwa: 19 Novemba, 2012 - Saa 08:13 GMT

Wapatanishi wa serikali ya Colombia wamewasili nchini Cuba kwa mazungumzo mahsusi ya amani na waasi wa FARC, yanayokusudia kukomesha mapigano ya miongo mitano huko Colombia.

Mazumgumzo hayo, yatakayofanywa mjini Havana, Cuba, ndiyo ya kwanza kufanywa katika miaka 10 iliyopita.

Mpatanishi mkuu wa serikali ya Colombia, Humberto de la Calle, alisema wakati ulikuwa umefika kwa waasi hao wa mrengo wa kushoto kuonyesha kwamba kweli walikuwa wanataka kusalimisha silaha zao, kwa dhati, na kujiunga na siasa kisheria kama chama halali.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.