Maelfu ya raia DRCongo wawatoroka waasi

Imebadilishwa: 19 Novemba, 2012 - Saa 07:47 GMT

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa huko mashariki mwa Jamuhuri ya Demokrasia ya Kongo wanasema kwamba hali ya kibanadamu inazidi kuzorota, huku makumi ya maelfu ya wananchi wakizidi kuwatoroka waasi.

Waasi wa M23 sasa wako kilomita chache tu kutoka mji mkuu wa mkoa wa Goma, hata baada ya kushambuliwa kwa helikopta za Umoja wa Mataifa.

Waasi hao wanasema kwamba hawakusudii kuuteka mji huo, lakini wakaazi wanahofia kwamba mji huo utatekwa wakati wowote.

Inasemekana kwamba baadhi ya wanajeshi wa Kongo waliokuwa wanailinda Goma wameshatoroka.

Umoja wa Mataifa umesema kwamba hautajibu mashambulizi ya waasi iwapo wataingia katika maeneo waishimo watu wengi, kwa kuhofia kuwajeruhi raia.

Kieran Dwyer, msemaji wa walinda amani hao, alisema, “Kwa sasa walinda amani wanajitahidi kuuthibiti mji wa Monigi, kilomita chache kutoka Goma, na vilevile kujaribu kuwalinda watu wengi waliotoroka – tunahisi kuwa takriban watu 60,000 wamefurushswa na mapigano haya.”

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.