Mlipuko ndani ya basi Tel Aviv

Imebadilishwa: 21 Novemba, 2012 - Saa 14:57 GMT

Takriban watu 17 wamejeruhiwa wawili kati yao wakiwa hali mahututi baada ya mlipuko wa bomu kutokea ndani ya basi mjini Tel aviv.

Picha za televisheni zimeonyesha basi likiwa limeegeshwa kwenye mtaa kutoka makao makuu ya ulinzi ya Israeli, huku madirisha yakiwa yamevunjwa na moshi ukitoka ndani ya basi hilo.

Msemaji wa waziri mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu, amethibitisha idadi hiyo ya majeruhi na kutaja shambulio hilo kuwa ni la ugaidi .

Hii inakuja baada ya mashambulio mengine ya makombora yaliyofanywa usiku na wanamgambo wa Israeli mjini Gaza, huku juhudi za kidiplomasia zikiendelea kujaribu kusitisha mapigano na Hamas.

Ndege za kijeshi, Helikopta na manuari za kijeshi zilihusika katika mapigano hayo.

Wanamgambo wa Israeli wanasema mashambulio mengi yalikuwa ni ya roketi za chini ya ardhi.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.