Mkuu wa polisi auawa Benghazi

Imebadilishwa: 21 Novemba, 2012 - Saa 11:41 GMT

Afisa mmoja mkuu wa usalama nchini Libya amepigwa risasi na kuuawa nje ya nyumba yake mjini Benghazi.

Wizara ya usalama wa ndani nchini humo imeelezea kuwa Bwana Faraj Al Deirsy, ambaye alikuwa mkuu wa polisi mjini humo, amefariki kutokana na majeraha ya risasi baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana.

Kumekuwa na visa vingi vya mauji mjini Benghazi katika siku za hivi punde.

Mnamo mwezi Septemba, balozi wa marekani mjini Benghazi aliuawa pamoja na wamarekani watatu katika ubalozi huo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.